Mnamo mwishoni mwa August mwaka huu 2014 nilifanya maamuzi ya kurudi shule. Nimepanga kusoma PhD mwakani. Maamuzi haya yamezingatia mambo mengi mno. Ila kubwa zaidi ni baada ya kujifanyia tathmini ya kuona ni kitu gani nina uwezo mkubwa wa kukifanya na nitakuwa na furaha kukifanya kitu hicho. Sekta ya elimu na hasa ufundishaji ni kitu kimo damuni, nina uwezo mkubwa wa kufundisha na ninakuwa na furaha nifundishapo. Hivyo sina budi kurudi shule na kuanza maisha mapya ya kuwa mwanafunzi wa PhD.
Nimeona ni vyema basi nioneshe safari hii naifanyaje katika kuomba vyuo na kupata udhamini. Hii itaweza kuwasaidia wadau wengi nanyi katika kujua uombaji unakuaje na ni jinsi gani ya kuandaa maombi yenye ushindani mkubwa.
- Mahala pa kusoma (Wapi?)
- Muda gani kuanza masomo (Lini?)
- Fani ya kusoma
- Udhamini wa elimu
- Ushindani katika mchakato wa uombaji vyuo na udhamini
- Masharti na vigezo katika uombaji
- Gharama za uombaji nk
Yaliyoorodheshwa hapo juu ni machache kati ya mengi ya kuzingatiwa. Nitachambua kila kimoja bila kufuata mtiririko wowote ule. Nitachukua mada moja baada ya nyingine na kuinyambua kuhakikisha ianeleweka kabla ya kwenda nyingine.
Kama msomaji, unaweza kuuliza swali wakakti wowote ule na nitaweza kujibu kwenye maoni yako. Lengo ni kuweka mtiririko huu kuwa kama jukwa la kusaidiana na kuwezeshana, kuelimishana na kupeana mbinu za ushindi.
Pia nitakuwa ninaweka video clips kadhaa nitakazokuwa naongelea mada hizi pia. Japo sio kila video itakuwa na maneno sawia na maandishi.
Karibu Sana
MAKULILO
3 Comments