Header

MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG YATIMIZA MIAKA 3

Libeneke La Nondozzz Latimiza Miaka Mitatu

Picha kushoto: Issa Michuzi (MICHUZI BLOG), Mrs. Marie A. Makulilo, Mr. Ernest B. Makulilo (MAKULILO BLOG)


MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG
INAADHIMISHA MIAKA 3.
BLOG ilianza kufanya kazi rasmi kuanzia JULY 2007. Mwezi huu JULY 2010 ni mwezi wa maadhimisho. Nipo katika hatua za mwisho za maboresho ya BLOG hii ambapo nitaongeza kipengele cha SCHOLARSHIP AUDIOS/VIDEOS ambapo nitakua najibu maswali ya wadau na kuweka dondoo za maandalizi ya mtu kuweza kupata scholarships North America na Western Europe.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kunisaidia katika mambo ya BLOG hususani MICHUZI (WWW.ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM) na DA SUBI (WWW.WAVUTI.COM) . Pia nawashukuru wale wote walionisaidia kuweza kuongea ktk ITV, TBC1 na TBC TAIFA kuhakikisha watu wengi wanajua taratibu za uombaji scholarships ughaibuni.

Naomba maoni yenu katika kuwezesha maboresho ya BLOG hii. Pia natoa wito kwa wengi kujiunga na SCHOLARSHIP FORUM WWW.SCHOLARSHIPNETWORK.NING.COM

ambapo unatakiwa ku-SIGN UP na kuwa member. Mara uwapo member utakuwa unapata scholarship updates kwenye E-MAIL INBOX yako kila ninapoweka taarifa kwenye FORUM na utakuwa na nafasi ya kuweka comment au kuuliza swali na kujibiwa papo hapo.

Post a Comment

6 Comments

Hongera kwa kutimiza miaka mitatu!!
SOSSY FORREAL said…
Safi sana kaka endeleza Harakati Kaka tuko Pamoja
mchanga saleh said…
ASNTE KAKA MUNGU ATAKULIPA HATUNA CHA KUKULIPA.
bob said…
nina diploma ya uhasibu je nitafanyje nipate sponsorship ya bachelor degree hapa hapa
Jacque said…
Hi,
Am 23 years old and i have completed my Bachelor degree in Accounting at the University of Dar es salaam July 2011. Am currently working as an auditor at this local auditing firm.
I am looking for a full MBA scholarship in the countries such as Canada, Denmark, Sweden..or any other country that may be able to offer me a full sponsorship.

Please if there is any open opportunities let me know.
MLELWA, Abel E said…
habari ya siku nyingi kidogo, kaka! niliwahi kuwasiliana na wewe kupitia blog yako mwaka jana, ulishauri mambo kadhaa kuhusu masters. kwa sasa ninamalizia shahada yangu ya awali katika Kiswahili katika chuo kikuu cha Dodoma. Kama ulivyonijulisha kwamba kupitia kozi yangu naweza kusoma masters, hivyo niliomba kusoma MA IN AFRICAN STUDIES huko UK (School of Oriental and African Studies, London University). nimekubaliwa na ninatakiwa kuanza chuo mwezi disemba mwaka huu. sasa, sijapata scholarship. naomba nisaidie mawazo au maeneo ambayo naweza kuomba scholarship na nikapata. ukihitaji nikutumie documents walizonitumia, basi nitafanya hivyo.

asante sana, nasubiri msaada wako.

Abel Mlelwa